Sera ya Faragha
Loss Recovery Partners (LRP) · lossrecoverypartnerztz.com · Dar es Salaam, Tanzania · Imesasishwa: Oktoba 2026
Tunaheshimu faragha yako. Ukurasa huu unaeleza taarifa tunazokusanya, kwa nini, tunazihifadhi wapi, na haki zako kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Tanzania (2022).
1. Taarifa tunazokusanya
- Kupitia fomu zetu (tovuti, Facebook/Instagram Lead Ads): jina, namba ya simu, na maelezo unayoandika mwenyewe (mfano unachotafuta).
- Kwa watumiaji wa mfumo wa LRP: taarifa za akaunti (jina, barua pepe, namba ya simu), na data ambazo biashara yako inaingiza kwenye mfumo (mauzo, stoo, wateja, wafanyakazi, ripoti).
2. Tunazitumia kwa nini
- Kuwasiliana nawe kuhusu ombi ulilotuma (simu, SMS, WhatsApp).
- Kukupatia na kuboresha huduma ya mfumo wa LRP, na kuhakikisha usalama wa akaunti.
- Kutimiza wajibu wa kisheria (mfano kumbukumbu za kodi).
Hatuuzi taarifa zako. Hatutumii taarifa zako kukutumia matangazo ambayo hukukubali kupokea.
3. Tunashiriki na nani
Tunatumia watoa huduma wa kiufundi kuendesha mfumo. Wanapata taarifa kwa kiasi kinachohitajika tu:
| Mtoa huduma | Kazi |
|---|---|
| Google Firebase | Kuhifadhi data ya mfumo |
| Netlify | Kuendesha tovuti na huduma za seva |
| Make | Kuhamisha leads kutoka Facebook kwenda mfumo wa LRP |
| Meta (Facebook / Instagram) | Kukusanya fomu za leads kwenye matangazo |
Baadhi ya watoa huduma hawa wako nje ya Tanzania; taarifa zako zinaweza kuhifadhiwa au kuchakatwa huko, kwa hatua za usalama zinazofaa.
4. Muda wa kuhifadhi
Tunahifadhi taarifa za leads kwa muda unaohitajika kuwasiliana nawe, kisha kuzifuta au kuzificha utambulisho. Taarifa za akaunti na kumbukumbu za kibiashara zinahifadhiwa kwa muda wa mkataba na muda wa sheria (kawaida miaka 5 kwa kumbukumbu za kodi).
5. Usalama
Tunatumia mawasiliano yaliyosimbwa (HTTPS), uthibitisho wa hatua mbili kwa watumiaji, na udhibiti wa nani anaweza kuona data kulingana na cheo. Hakuna mfumo wa mtandaoni ulio salama kwa 100%, lakini tunaendelea kuuboresha.
6. Haki zako
- Kuomba kuona taarifa tulizonazo kukuhusu.
- Kuomba zisahihishwe au zifutwe.
- Kupinga au kuomba tuache kuzitumia kwa masoko, wakati wowote.
- Kuwasilisha malalamiko kwa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) ukiona haki zako hazijaheshimiwa.
Tuma ombi kwa kutumia simu 0749 488 769 au 0612 085 882, WhatsApp 0612 085 882, au barua pepe lossrecoverypartnerztz@gmail.com. Tutajibu ndani ya siku 7 za kazi.
7. Mabadiliko
Tukibadilisha sera hii, tutaweka tarehe mpya juu ya ukurasa huu.